Takwimu za Pato la Taifa
Takwimu za kiuchumi zinatumika kubainisha utekelezaji wa shughuli mbalimbali za kiuchumi katika nchi. Chanzo kikuu za takwimu za kiuchumi ni taarifa za kiutawala. Vyanzo vingine ni: sensa, tafiti na kwa kipindi cha hivi karibuni “big data” inayohusisha taarifa za biashara katika maduka ya supermarket, vituo vya mafuta n.k. kimekuwa ni chanzo kipya chenye taarifa nyingi zinazofaa kuandaa takwimu za kiuchumi. Takwimu za kiuchumi huwasilishwa kwa mtiririko unaojumuisha miaka miaka iliyopita ambapo pia zinatumika kutayarisha maoteo ya kipindi kijacho. Takwimu za kiuchumi zinazotayarishwa na kusambazwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu zinajumuisha: Takwimu za Pato la Taifa, Takwimu za Viwanda na Ujenzi; Takwimu za Kilimo, Takwimu za Biashara ya Nje, Usafirishaji, Utalii na uhamaji. Kwa taarifa zaidi wasiliana nasi kupitia anuani ya barua pepe Adella.ndesangia@nbs.go.tz