Takwimu za Mazingira
Uzalishaji wa Ripoti ya Taifa ya Takwimu za Mabadiliko ya Tabianchi, 2019 (NCCSR, 2019) ni juhudi za ushirikiano kati ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu, (NBS); Kamati ya Ufundi ya Taifa ya Takwimu za Mazingira (NTWG), inayoundwa na wajumbe kutoka Wizara, Idara na Wakala mbalimbali (MDAs); Shirika la Ushirikiano wa Kimataifa wa Ujerumani, (GIZ); Idara ya Takwimu ya Umoja wa Mataifa (UNSD); Ushirikiano wa Kimataifa wa Takwimu za Maendeleo Endelevu, (GPSDD) na Mpango wa Mazingira wa Umoja wa Mataifa, UNEP. Rasilimali fedha kwa ajili ya kazi hii zilitolewa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, (URT); Shirika la Ushirikiano wa Kimataifa la Ujerumani, (GIZ) na Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP).