Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Taifa ya Takwimu

Takwimu kwa Maendeleo
Takwimu za Jinsia

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar zinaamini kwa dhati kwamba masuala ya jinsia ni muhimu kwa maendeleo katika ngazi zote za jamii. Kwa sababu hii, Tanzania ilifanya utafiti wa SIGI ambao ulihusisha masuala ya jinsia, mila, desturi na tamaduni za Tanzania. Dhamira ya Tanzania ya kufanya utafiti huu ni kuelewa changamoto ambazo bado zinazuia uwezeshaji wa wanawake na kukwamisha usawa wa kijinsia. Matokeo ya utafiti wa SIGI nchini Tanzania yanaonesha hali ya kuridhisha. Marekebisho ya sera na sheria yanayolenga usawa wa kijinsia yamechangia kuboresha usawa wa kijinsia wakati washirika wa kitaifa na kimataifa pia wamechukua jukumu katika kutekeleza sera ya jinsia na uhamasishaji wa usawa wa kijinsia katika jamii. Ni matumaini yetu kwamba matokeo ya utafiti na ripoti ya SIGI yataendelea kutumika katika utengenezaji na uhuishaji wa sera, kuharakisha mabadiliko ya kuelekea usawa wa kijinsia na kusaidia kutimiza matarajio ya kitaifa na kimataifa ya maendeleo endelevu kwa wote.