Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Taifa ya Takwimu

Takwimu kwa Maendeleo
Mfumo wa Taarifa za Kijiografia (GIS)

GIS ni mfumo wa mawasiliano wa taarifa za kijiografia ambao msingi wake kubwa ni kuhifadhi, kukusanya, kuchambua, kuonesha na kusambaza taarifa husika kwa watumiaji kwa ajili ya kutumika katika kufanya maamuzi yenye ushahidi sahihi kitakwimu. Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) ilianza kutumia mfumo huu tangu mwaka 2002 ambapo umuhimu wa matumizi ya mfumo huu umedhihirisha kuwa, 1) Mfumo huu unatoa data/takwimu zinazohitajika kwa uhalisia na kwa wakati; 2) Unatumika katika kuboresha takwimu kwa gharama nafuu na kwa wakati; 3) Unarahisisha ukusanyaji wa takwimu kwa haraka na wepesi zaidi; 4) Unawezesha kutumika na kuonesha takwimu ki taswira (visualization); 5) Unasaidia sana katika suala la ufuatiliaji na tathmini; 6) Unatumika katika kubaini mwenendo na mabadiliko yanayotokea katika sura ya eneo husika; na 7) Uwezesha kuelewa kwa urahisi mtu yeyote mwenye taaluma tofauti au asie na taaluma yeyote, kufahamu kwa urahisi matumizi ya takwimu za kijiografia. Matumizi ya mfumo huu, hasa katika mazoezi makubwa likiwemo zoezi la Sensa ya Watu ambalo hugharimu fedha nyingi, uliiwezesha NBS kutumia gharama ndogo wakati wa zoezi la kutenga maeneo ya kuhesabia watu kwa kuwa, ililazimu kutumia watu wachache wakati wa kufanya kazi hiyo. Aidha, wakati wa utekelezaji wa zoezi tajwa, hakukuwa na matumizi ya karatasi na mwendendo wa kazi husika taarifa zake zilipatikana kwa wakati (real time based) na kutumwa moja kwa moja kwenye Seva (Sever).

Mada Zinazohusiana