Muhtasari wa Takwimu za Msingi
Chapisho la Muhtasari wa Takwimu uandaliwa kila mwaka na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) linatoa muhtasari wa takwimu mbalimbali za Kiuchumi na Kijami. Takwimu zilizopo kwenye chapisho zinajumuisha taarifa za kitakwimu za viashiria muhimu vya mwaka 2023 na taarifa nyingine ambazo ni za hivi karibuni. Takwimu za mwaka 2023 ni kama zifuatazo; takwimu za mazingira na mabadiliko ya tabianchi; muundo wa bunge hadi Desemba; makadirio ya idadi ya watu Tanzania Bara, takwimu za hesabu za taifa, kilimo- uzalishaji wa mazao ya biashara, takwimu za viwanda, takwimu za ujenzi, takwimu za biashara, takwimu za uchukuzi na mawasiliano, sarafu na benki hadi mwishoni mwa Desemba, elimu shule za msingi za umma na binafsi, takwimu za afya, hoteli na hifadhi za taifa, takwimu za bei za rejareja, takwimu za uhalifu, na utafiti wa athari za VVU Tanzania. Aidha, chapisho hili pia lina taarifa za takwimu za hivi karibuni kuhusiana na ajira 2020/21, takwimu za uwekezaji 2022, takwimu za utafiti wa mapato na matumizi ya kaya binafsi 2017-2018, na takwimu za orodha ya shughuli za kiuchumi na kijamii 2023/2024.