Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Taifa ya Takwimu

Takwimu kwa Maendeleo
Takwimu za Msingi Tanzania

Kitabu cha Takwimu za Msingi cha Tanzania kinatoa picha ya hali halisi ya mwenendo katika nyanja za uchumi, jamii, mazingira na siasa. Kitabu hiki kinatoa muhtasari wa takwimu kutoka vyanzo mbalimbali vya taarifa kutoka machapisho ya takwimu rasmi yanatolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Wizara, Idara na Wakala nyingine za Serikali. Taarifa za takwimu zilizowasilishwa ni muhimu kwa kupanga mipango, kufuatilia na kutathimini programu mbalimbali za maendeleo katika ngazi zote za kiutawala.